The word of today



MAOMBI-1
Utangulizi:
Maombi hutusaidia kumjua Mungu, kumwamini na kutoa majibu ya mahitaji yetu kutoka kwake. Mtu anayedumu katika kuomba hupata nguvu za kumuwezesha kuishi maisha ya ushindi.

Maombi ni nini?
Kuomba ni kuongea na kumsikiliza Mungu, Unamletea mahitaji yako na unaamini kwamba atayajibu. Maombi ni pamoja na kumshukuru Mungu kwa aliyokutendea, kumsifu jinsi alivyo na kumuabudu. 
Kuomba ni kueleza shauku na mahitaji yetu katika ahadi ya Mungu kwa mwanadamu, katika unyenyekevu mwingi huku tukiamini kuwa tukiombacho tutakipata kupitia kwa Yesu Kristo kwa ajili ya kutukuzwa Mungu na kwa kutatua matatizo yetu. Kuomba ni kutafuta msaada kutoka kwa Mungu katika mambo ambayo ni nje ya uwezo wetu wa kimwili.
Maombi ni kuomba na kupokea kutoka kwa Mungu.

Kwa nini tuombe? (Luke 11: 1, 9-13)
Kuomba hutuwezesha kuweka matumaini yetu kwa Mungu na kumuacha afanye kwa niaba yetu/ Ni hali ya kumtegemea Mungu kwani ametuagiza tumuite naye atatuitikia.
Namna ya kuomba
Wanafunzi wa Yesu waliomba wafundishwe namna ya kuomba baada ya kugundua kuwa hata Yesu alikuwa akijitenga na kuomba.
Katika Luka 11: 2-4 Yesu aliwapa wanafunzi vipengele vya kuomba vikiwa ni pamoja na:
·Kumsifu
·Kutaka mapenzi yake yatimizwe
·Kumshukuru
·Kusamehe waliotukosea
·Kuomba msamaha (Zab,66:18)
·Kuomba mahitaji yetu ya kumwili, kinafsi na kiroho(Yohana 16:24) Kila kitu omba kwa jina la Yesu
· Kuomba tusiangukie majaribuni
· Kuomba atuokoe na mwovu shetani
Mungu anajibu maombi pale mwamini anapoomba kwa uaminifu kwa imani.

2 comments:

  1. OUR MOST SOVEREIGN GOD ALWAYS SEEKETH THE TRUE WORSHIPERS TO WORSHIP HIM IN SPIRIT AND TRUTH

    ReplyDelete