Monday, April 2, 2018

TAMASHA KUBWA LA KUSIFU NA KUABUDU - MCRC

Leo tumekuwa na Tamasha kubwa sana la kusifu na kuabudu lililofanyika hapa kanisani MCRC


Tamasha hili lililobeba jina la Amefufuka (He is Risen). lilikuwa la kipekee sana ambapo watu wengi walijumuika pamoja nasi kumsifu na kumshangilia Mungu kwa kuwa ameishinda mauti.

(Mchungaji Godwin Mujaki (kushoto) -  Mwimbaji Bomby Johnson (Kulia))
    
Tamasha hili lilihudumiwa na waimbaji mbali mbali, akiwemo Bomby Johnson
(Pichani ni Mwimbaji Bomby Johnson akihudumu)

Baadhi ya washirika na wageni mbali mbali wakimsifu Mungu kwenye Tamasha la leo

Walawi Praise Team, wakiongoza sifa katika Tamasha la leo

Pichani ni baadhi ya watu walioenda mbele kumsifu Mungu

Vijana wakimsifu Mungu kwenye Tamasha MCRC


Tamasha hili liliambatana na maombezi ambapo watu wenye shida mbali mbali waliombewa na Mungu alikutana na mahitaji ya kila mmoja

Maombi na maombezi yakiwa yanaendelea kwenye Tamasha kubwa la kusifu na kuabudu


Mchungaji kiongoziwa TAG - Msewe, Mchungaji Godwin Mujaki akiongoza maombi na maombezi mara baada ya ibada ya kusifu na kuabudu