Saturday, April 4, 2015

KUTENGENEZA TABIA NJEMA

Tunamshukuru Mungu Jumapili ya leo tumekuwa na ibada njema sana iliyoendeshwa na mtumishi wa Mungu Andrea Benedictor. Mungu alimtumia kwa namna ya kipekee. Ujumbe aliofundhisha Jumapili ya leo ni "KUTENGENEZA TABIA NJEMA"
Maana ya tabia
 Mazoea(kufanya jambo mara kwa mara na baadaye inakuwa sehemu ya maisha)inakuwa ngumu kuacha.
Mwenendo-staili ya maisha,
Desturi –tabia ya kurithi katika jamii ya mahali fulani.Mfano. Wachaga wana tabia ya kupenda fedha,Wahaya wanapenda kusoma
Wanasaikolojia
Tabia ni matendo,mienendo au hulka zinazoweza kuonekana wazi,kupimwa na hata kuchunguzika kwa misingi ya kisayansi(tafiti) na kawaida.
Ingawa misingi ya tabia zote ni mawazo,imani,fikra na mitazamo isiyoonekana LAKINI Matokeo yake ni kuonekana kwa vitendo.
Hivyo mawazo ya aina fulani uendelea kwenye ufahamu wa mtu na matokeo yake ni  vitendo.1Kor.15:33 “Msidanganyike,mazungumzo mabaya,huharibu tabia njema)
Ki-Biblia
Tabia mbaya inaitwa Mambo ya mwilini,tabia ya asili,ya dunia,kibinadamu,kishetani,mataifa.
Yakobo 3:15
(Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya dunia, ya tabia ya kibinadamu, na Shetani.)Tabia nzuri inaitwa Tabia ya Rohoni,Ki-ungu.Mara nyingi huioni kwako bali watu wengine ndio wanaiona.
I.TABIA MBAYA HUZAA MATATIZO MENGI
 1. Jamii inakutenga,inakukimbia
2. Kukosa fursa(Kazi,kuinuliwa-promotion,kufukuzwa kazi,kukosa tenda)
3.Kuzuia maendelea-Kwenye nafasi fulani,Mkuu wa Idara fulani(“achana idara”)
4.Kuwa kwazo-Kila siku unakuwa unakwaza watu,ni wewe tu unayesababisha
Matatizo.Watu wanaanza kufunga na kuomba kwa ajili ya makwazo yako
5.Unajizuilia Baraka za Mungu.Mungu akikuangalia akubariki kwa Baraka zake,
ili ufanyike jibu kwa watu,anaona tabia ya ubinafsi,uchoyo,Anaona madhara
hasi Badala ya watu kubarikiwa anaona wananyanyasika
6. Dharau na fedheha.Ukiwa na tabia mbaya utadharaulika na jamii inayokuzunguka
III:ACHA TABIA MBAYA
A.Omba Mungu akufunulie tabia zako mbaya.Uliza mtu wako wa karibu akueleze.
B: Zichukie tabia mbaya ulizo nazo
C: Kubali Ushauri
B.Amua kuanza kuishi maisha ya kupendeza.
Wafilipi.4:8
Hatimaye, ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye kupendeza, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote, yatafakarini hayo.
C:Omba uwezesho wa Roho Mtakatifu.
Warumi 12:1-2
1 Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana.
 2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.






No comments:

Post a Comment