Sunday, November 26, 2017

ELEWA NGUVU YA TABIA, NA UKUZE TABIA NJEMA - MCH:GODWIN MUJAKI

Siku ya leo ilikuwa ya baraka sana, baada ya Mungu kumtumia mchungaji kiongozi wa kanisa la Msewe Christian Revival Centre , Mchungaji Godwin Mujaki katika kufundisha Somo zuri la Tabia.

(Pichani ni Mchungaji Godwin Mujaki akihubiri.)

Katika mafundisho yake, alitolea mifano mbali mbali ya tabia za baadhi ya watu kwenye biblia, ikiwemo tabia ya Yesu, ambapo alisema kuwa Yesu alikuwa (Mtu wa ibada (Luka 4:16)  pamoja na (Mtu wa maombi (Yohana 18:1-2).

(Pichani ni washirika wakisikiriza neno la Mungu)


VITU VYA KUFAHAMU KUHUSU TABIA
1.Tabia yaweza kuwa mbaya au nzuri na pia tabia inaweza ikawa ya kiroho au ya asili.
2. Ni kitendo kinachorudiwa kwa urahisi pasipo kufikilia au kupanga kukifanya
3. Tabia mbaya huongoza katika kushindwa,uwe unajua au haujui
4. Tabia nzuri huongoza kwenye kushinda ikiwa muhusika anajua au hajui
5. Tabia nzuri ni ngumu kuitengeneza, ilanirahisi kukaa nazo
6. Tabia mbaya ni rahisi kuzitengeneza ila ni ngumu kukaa nazo
7. Unapokuwa na tabia njema, ni lazima uwe mlinzi wa tabia hiyo.
1 Wakorintho 15:33


Pichani ni Mchungaji Godwin Mujaki (kushoto) pamoja na mtafsiri wake, Mchungaji Denis Bashurura.


VITU VYA KUZINGATIA
1.Upo hivyo kama ulivyo kutokana na Tabia
2.Tabia nikitu unafanya bila kukusudia na bila kujua
3. Tabia hutokea kwa mtu, kwa kupanga, kwa kupania na kwakujizoesha kufanya jambo hilo hilo bila kukatishwa na mtu
4.Daniel alikuwa na tabia ya kuomba sirini (Daniel 6:10)
5. Imani iliyojengwa juu ya tabia, ni imani isiyoshindwa.


HAKIKA TULIBARIKIWA SANA. KARIBU SANA MSEWE CHRISTIAN REVIVAL CENTRE. 
Mawasiliano : +255 752 636 641


WOTE MNAKARIBISHWA.








3 comments:

  1. Mungu awabariki wote mlio sikiliza mafundisho hayo. Iweni watendaji wa neno na wala si wasikilizaji tu

    ReplyDelete
  2. Nimebarikiwa sana pamoja na somo ni LA mda sana ila naenda kuwa mwalimu wa wengine

    ReplyDelete
  3. Somo zuri lina tuimarisha.

    ReplyDelete