Tuesday, October 17, 2017

BWANA NIFANYE KUWA LANGO LA KUPITISHIA BARAKA ZAKO

Hivi ndivyo tulivyo hitimisha Jumapili yetu kwa somo zuri ambalo Mungu alimtumia mtumishi wake, askofu Chrisantu Siame, alivyo kuja kuhubiri katika kanisa la Msewe Christian Revival Centre.


Pichani ni Mchungaji kiongozi kwa kanisa la MSEWE CHIRSTIAN REVIVAL CENTRE, Mchungaji GODWIN MUJAKI, akimkaribisha Askofu CHRISANTU SIAME.



Pichani, ni Mchungaji Godwin Mujaki na Mke wake Scola Mujaki, pamoja na Mchungaji Chrisantu Siame, na mke wake, nyuma, ni baadhi ya Wachungaji wasaidizi, na wazee wa kanisa. Pamoja wakimtukuza Mungu.



Pichani, ni Askofu Chrisantu Siame, akifundisha somo kwa mifano. mbali mbali

Pichani, ni Askofu Chrisantu Siame, akimshukuru Mungu kwa watu walivyojitoa katika ibada ya leo. na kuwaombea Mungu aende kukutana na haja za mioyo yao.


HAKIKA TULIBARIKISWA SANA. 
USIKOSE JUMAPILI IJAYO KANISANI 
MSEWE CHRISTIAN REVIVAL CENTRE.


Sunday, October 8, 2017

MATUKIO YA TAMASHA KUBWA LA KUSIFU NA KUABUDU , "SHANGWE NA ZISIKIKE"

Tunamshukuru Mungu, siku ya leo tumekuwa na Tamasha kubwa la kusifu na kuabudu , lililobeba jina la "SHANGWE NA ZISIKIKE"


Timu ya waimbaji , ijulikanalo kama "WALAWI". Wakielekea madhabahuni.




Timu ya WALAWI, ikihudumu madhabahuni katika tamasha kubwa la kusifu na kuabudu


Pichani, ni Kwaya ya Vijana, ijulikanayo kama "GOOD NEWS BRINGERS", ikihudumu katika Tamasha kubwa la kusifu na kuabudu.


PICHANI: ni Mchungaji kiongozi wa kwaya ya WALAWI, akiwapongeza watu kwa kuhudhuria kwa wingi.



Pichani: Mchungaji kiongozi wa kanisa la Msewe Christian Revival Centre, Mchungaji Godwin Mujaki. akimuabudu Mungu katika Tamasha kubwa la Kusifu na Kuabudu.


Pichani: Mama mchungaji wa kanisa la Msewe Christian Revival Centre, Mama Mchungaji Scolla Mujaki. akimuabudu Mungu katika Tamasha kubwa la Kusifu na Kuabudu.


Pichani ni baadhi ya watumishi wa Mungu wakikemea pepo, katika Tamasha kubwa la Kusifu na kuabudu.




Hakika tulimuona Mungu katika tamasha hili, usikose kila jumapili kufika kanisani Msewe Christian Revival Centre. 

WATU WOTE MNAKARIBISHWA.