Monday, April 2, 2018

TAMASHA KUBWA LA KUSIFU NA KUABUDU - MCRC

Leo tumekuwa na Tamasha kubwa sana la kusifu na kuabudu lililofanyika hapa kanisani MCRC


Tamasha hili lililobeba jina la Amefufuka (He is Risen). lilikuwa la kipekee sana ambapo watu wengi walijumuika pamoja nasi kumsifu na kumshangilia Mungu kwa kuwa ameishinda mauti.

(Mchungaji Godwin Mujaki (kushoto) -  Mwimbaji Bomby Johnson (Kulia))
    
Tamasha hili lilihudumiwa na waimbaji mbali mbali, akiwemo Bomby Johnson
(Pichani ni Mwimbaji Bomby Johnson akihudumu)

Baadhi ya washirika na wageni mbali mbali wakimsifu Mungu kwenye Tamasha la leo

Walawi Praise Team, wakiongoza sifa katika Tamasha la leo

Pichani ni baadhi ya watu walioenda mbele kumsifu Mungu

Vijana wakimsifu Mungu kwenye Tamasha MCRC


Tamasha hili liliambatana na maombezi ambapo watu wenye shida mbali mbali waliombewa na Mungu alikutana na mahitaji ya kila mmoja

Maombi na maombezi yakiwa yanaendelea kwenye Tamasha kubwa la kusifu na kuabudu


Mchungaji kiongoziwa TAG - Msewe, Mchungaji Godwin Mujaki akiongoza maombi na maombezi mara baada ya ibada ya kusifu na kuabudu

Sunday, January 14, 2018

USILIE MWANGALIE YESU - MCHUNGAJI DAVID MWAKAJINGA

Leo tumekuwa na ibada ya kipekee, ni baada ya kutembelewa na ugeni mkubwa kutoka kanisa la TAG Buguruni.

(Pichani ni Mchungaji David Mwakajinga akihubiri)

Watu wengi walibarikiwa kwa somo zuri la USILIE MWANGALIE YESU. 

 (Pichani ni Mchungaji David Mwakajinga akiwaombea waumini)

(Pichani ni Mchungaji Godwin Mujaki akiwaombea washirika)

 Kwaya ya Eden B  kutoka TAG BUGURUNI IKIHUDUMU

                 Washirikika wakisikiliza neno la Mungu
  Timu ya kusifu na kuabudu ya walawi ikihudumu

  Washirikika wakisikiliza neno la Mungu

                  Timu ya kusifu na kuabudu ya walawi ikihudumu

Mchungaji David Mwakajinga na mke wake, pamoja na Mchungaji Godwin Mujaki wakimtukuza Mungu kwa pamoja


Watumishi wa Mungu wakitoa pepa

            Baadhi ya watu waliokoka katika ibada ya leo