Sunday, November 26, 2017

ELEWA NGUVU YA TABIA, NA UKUZE TABIA NJEMA - MCH:GODWIN MUJAKI

Siku ya leo ilikuwa ya baraka sana, baada ya Mungu kumtumia mchungaji kiongozi wa kanisa la Msewe Christian Revival Centre , Mchungaji Godwin Mujaki katika kufundisha Somo zuri la Tabia.

(Pichani ni Mchungaji Godwin Mujaki akihubiri.)

Katika mafundisho yake, alitolea mifano mbali mbali ya tabia za baadhi ya watu kwenye biblia, ikiwemo tabia ya Yesu, ambapo alisema kuwa Yesu alikuwa (Mtu wa ibada (Luka 4:16)  pamoja na (Mtu wa maombi (Yohana 18:1-2).

(Pichani ni washirika wakisikiriza neno la Mungu)


VITU VYA KUFAHAMU KUHUSU TABIA
1.Tabia yaweza kuwa mbaya au nzuri na pia tabia inaweza ikawa ya kiroho au ya asili.
2. Ni kitendo kinachorudiwa kwa urahisi pasipo kufikilia au kupanga kukifanya
3. Tabia mbaya huongoza katika kushindwa,uwe unajua au haujui
4. Tabia nzuri huongoza kwenye kushinda ikiwa muhusika anajua au hajui
5. Tabia nzuri ni ngumu kuitengeneza, ilanirahisi kukaa nazo
6. Tabia mbaya ni rahisi kuzitengeneza ila ni ngumu kukaa nazo
7. Unapokuwa na tabia njema, ni lazima uwe mlinzi wa tabia hiyo.
1 Wakorintho 15:33


Pichani ni Mchungaji Godwin Mujaki (kushoto) pamoja na mtafsiri wake, Mchungaji Denis Bashurura.


VITU VYA KUZINGATIA
1.Upo hivyo kama ulivyo kutokana na Tabia
2.Tabia nikitu unafanya bila kukusudia na bila kujua
3. Tabia hutokea kwa mtu, kwa kupanga, kwa kupania na kwakujizoesha kufanya jambo hilo hilo bila kukatishwa na mtu
4.Daniel alikuwa na tabia ya kuomba sirini (Daniel 6:10)
5. Imani iliyojengwa juu ya tabia, ni imani isiyoshindwa.


HAKIKA TULIBARIKIWA SANA. KARIBU SANA MSEWE CHRISTIAN REVIVAL CENTRE. 
Mawasiliano : +255 752 636 641


WOTE MNAKARIBISHWA.








Sunday, November 12, 2017

IBADA KUBWA YA SHUKRANI KWA AJILI YA VYOMBO VYA KIMATAIFA.

Tunamshukuru Mungu tumekuwa na ibada kubwa ya shukrani kwa ajili ya vyombo vikubwa sana vya injili.

Pichani ni mchungaji Godwin Mujaki akiwa anahubiri katika ibada kubwa ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya vyombo vipya vya kisasa vya injili.

Pichani ni mama mchungaji Scolla Mujaki akiwa amefurahia uwepo wa Bwana katika ibada kubwa ya leo.


Mchungaji Godwin Mujaki (kushoto), akimtambulisha Mmishenari Macha mbele ya hadhara ya waliohudhuria tukio kubwa la leo


Mafundi mitambo wakielekezana baadhi ya vitu katika tukio kubwa la leo.


Muimbaji wa kitaifa , Mhe, Ambwene Mwasongwe, akimtukuza Mungu katika tukio kubwa la leo.


Tukio la leo liliambatana na kuwapokea wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliojiunga vyuo mbali mblai jijini Dar es Salaam , kila mwanafunzi alipewa zawadi ya biblia kubwa , ambayo itamsaidia awapo masomoni.


Pichani ni Professor Mato kutoka chuo kikuu cha Ardhi, akikaribishwa kuzungumza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliokuja Dar kuanza masomo yao.


Wageni kutoka korea, wakiimba wimbo.


Askofu kutoka Korea, akihubiri kwa kutumia mifano mbali mbali.


Wachungaji kutoka Msewe pamoja na Baraza la wazee wakipiga picha ya pamoja na wageni kutoka Korea.



Waimbaji kutoka nchi mbali mbali, (Argentina, Mexico, Korea, Thailand , Malawi, Kenya)
 wakijumuika kwapamoja na washirika wa msewe, katika kumsifu Mungu kwa ajili ya Vyombo vipya vya injili.


HAKIKA TULIBARIKIWA SANA. KARIBUNI SANA MSEWE CHRISTIAN REVIVAL CENTRE.