Saturday, December 16, 2017

MKESHA WA VIPAJI - JIGUNDUE KIPAJI CHAKO

Tunamshukuru Mungu, tumekuwa na mkesha mkubwa, uliowakutanisha wanavyuo wote waliopo Dar Es Salaam kwa pamoja katika tukio kubwa la Kugundua vipaji walivyonavyo.

(Pichani ni wanafunzi wa vyuo mbali mbali Dar Es Salaam, wakimsifu Mungu)

Pia, katika tukio hili la usiku wa kujigundua,  (Talent ovenight Exhibition,), tulikuwa na somo zuri kutoka kwa mchungaji Michael marabeja, 

Pichani ni mchungaji Michael Malabeja Akihubiri

Mchungaji Michael alihubiri somo lililobeba kichwa cha "Vitu ambavyo vinaweza kuchangia usifikie kiwango ambacho Mungu amekuwekea ndani yako".

aliorodhesha baadhi ya vitu hivyo kama

1. Ukosefu wa Utii kwa kitu Mungu alichoweka ndani yako.
2. Hofu ya kushindwa kufanikiwa
3. Kukata tamaa (Kila kitu kizuri kinahitaji uvumilivu)

(Wanafunzi wa vyuo wakimsikiliz mchungaji Michael akiwa anahubiri)

4. Mtazamo"Hakuna mtu anaweza akakuhukumu katika jambo zaidi ya wewe mwenyewe na neno la Mungu"
5. Mtazamo cha hasi (Kuhairisha mambo unayotaka kuyafanya kutokana na mtazamo hasi)
6. Kushindwa mara kwa mara
7. Mtazamo(Mrejesho) wa watu wengine juu ya maisha yako.
8. Kupoteza Muelekeo wa jambo ulilokusudia kulifanya
(1kor 6:12)
9. Kuridhika na mafanikio madogo madogo
(uwezo ni wewe ulivyotakiwa kuwa, ila bado haujafikia ulivyotakiwa kuwa)
10.Kuwa katika mazingira yasiyofaa
11. Kujilinganisha na watu wengine
12. Dhambi

Mchungaji Michael Malabeja, akiwaombea wanafunzi walioamua kuokoka


Katika mkesha huu, kulikuwa na waimbaji mbali mbali waliojumuika pamoja nasi katika usiku wa kujigundua.

 Mwimbaji Bale John akimtukuza Mungu katika mkesha wa kujigundua

 Mwimbaji Sarah Ndosi akimtukuza Mungu katika mkesha wa kujigundua
   


Monday, December 11, 2017

FANYA MAAMUZI SAHIHI - MR. EMMANUEL WAMBURA

Tunamshukuru Mungu Jumapili hii tumekuwa na ibada ya baraka sana, Mungu alimtumia Mtumishi wake Mr, Emmanuel Wambura, katika kutukumbusha Somo la Kufanya maamuzi sahihi.

 (Pichani ni Mr. Emmanuel Wambura akihubiri)

Mr. Wambura, akiwa na Mtafsiri wake Mchungaji Michael Malabeja, aliwakumbusha washirika, kuwa katika kila jambo wanalolifanya lazima kuna maamuzi mawili yapo mbele yanatakiwa kuchaguliwa, either, maamuzi mazuri, au maamuzi mabaya.

(Pichani ni Mr. Emmanuel Wambura na Mchungaji Michael Malabeja wakihubiri)

Mhubiri alitumia maandiko kutoka kitabu cha Mwanzo 4:1-7 katika kufikisha ujumbe aliotumiwa na Mungu

Mwanzo 4:1-7
 1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana.
 2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.
 3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.
 4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
 5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
 6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
 7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.

 (Pichani, ni washirika wakisikiliza neno la Mungu)


Mchungaji kiongozi, wa kanisa la Msewe Christian Revival Centre, mchungaji Godwin Mujaki alihitimisha kwa kumshukuru Mr. Emmanuel Wambura kwa kuitikia wito wa kufikisha ujumbe Mungu aliokusudia na kusisitiza washirika wautendee kazi ujumbe huo.

(Pichani ni Mchungaji Godwin Mujaki akimshukuru Mr. Emmanuel Wambura.)

Mchungaji Godwin Mujaki, aliwaombea watu wenye matatizo mbali mbali waliohitaji mkono wa Mungu kuingilia kati katika maisha yao.

(Washirika wakifanyiwa maombi)

HAKIKA TULIBARIKIWA SANA KATIKA IBADA HII. KARIBU SANA MSEWE CHRISTIAN REVIVAL CENTRE, KWA MCHUNGAJI GODWIN NA SCOLLA MUJAKI.

KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA NAMBA  :   0752 636641