Wednesday, November 15, 2017
Sunday, November 12, 2017
IBADA KUBWA YA SHUKRANI KWA AJILI YA VYOMBO VYA KIMATAIFA.
Tunamshukuru Mungu tumekuwa na ibada kubwa ya shukrani kwa ajili ya vyombo vikubwa sana vya injili.
Pichani ni mama mchungaji Scolla Mujaki akiwa amefurahia uwepo wa Bwana katika ibada kubwa ya leo.
HAKIKA TULIBARIKIWA SANA. KARIBUNI SANA MSEWE CHRISTIAN REVIVAL CENTRE.
Pichani ni mchungaji Godwin Mujaki akiwa anahubiri katika ibada kubwa ya kumshukuru Mungu kwa ajili ya vyombo vipya vya kisasa vya injili.
Pichani ni mama mchungaji Scolla Mujaki akiwa amefurahia uwepo wa Bwana katika ibada kubwa ya leo.
Mchungaji Godwin Mujaki (kushoto), akimtambulisha Mmishenari Macha mbele ya hadhara ya waliohudhuria tukio kubwa la leo
Mafundi mitambo wakielekezana baadhi ya vitu katika tukio kubwa la leo.
Muimbaji wa kitaifa , Mhe, Ambwene Mwasongwe, akimtukuza Mungu katika tukio kubwa la leo.
Tukio la leo liliambatana na kuwapokea wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliojiunga vyuo mbali mblai jijini Dar es Salaam , kila mwanafunzi alipewa zawadi ya biblia kubwa , ambayo itamsaidia awapo masomoni.
Pichani ni Professor Mato kutoka chuo kikuu cha Ardhi, akikaribishwa kuzungumza na wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliokuja Dar kuanza masomo yao.
Wageni kutoka korea, wakiimba wimbo.
Askofu kutoka Korea, akihubiri kwa kutumia mifano mbali mbali.
Wachungaji kutoka Msewe pamoja na Baraza la wazee wakipiga picha ya pamoja na wageni kutoka Korea.
Waimbaji kutoka nchi mbali mbali, (Argentina, Mexico, Korea, Thailand , Malawi, Kenya)
wakijumuika kwapamoja na washirika wa msewe, katika kumsifu Mungu kwa ajili ya Vyombo vipya vya injili.HAKIKA TULIBARIKIWA SANA. KARIBUNI SANA MSEWE CHRISTIAN REVIVAL CENTRE.
Tuesday, October 17, 2017
BWANA NIFANYE KUWA LANGO LA KUPITISHIA BARAKA ZAKO
Hivi ndivyo tulivyo hitimisha Jumapili yetu kwa somo zuri ambalo Mungu alimtumia mtumishi wake, askofu Chrisantu Siame, alivyo kuja kuhubiri katika kanisa la Msewe Christian Revival Centre.
Pichani ni Mchungaji kiongozi kwa kanisa la MSEWE CHIRSTIAN REVIVAL CENTRE, Mchungaji GODWIN MUJAKI, akimkaribisha Askofu CHRISANTU SIAME.
Pichani, ni Mchungaji Godwin Mujaki na Mke wake Scola Mujaki, pamoja na Mchungaji Chrisantu Siame, na mke wake, nyuma, ni baadhi ya Wachungaji wasaidizi, na wazee wa kanisa. Pamoja wakimtukuza Mungu.
Pichani, ni Askofu Chrisantu Siame, akifundisha somo kwa mifano. mbali mbali
Pichani, ni Askofu Chrisantu Siame, akimshukuru Mungu kwa watu walivyojitoa katika ibada ya leo. na kuwaombea Mungu aende kukutana na haja za mioyo yao.
HAKIKA TULIBARIKISWA SANA.
USIKOSE JUMAPILI IJAYO KANISANI
MSEWE CHRISTIAN REVIVAL CENTRE.
Sunday, October 8, 2017
MATUKIO YA TAMASHA KUBWA LA KUSIFU NA KUABUDU , "SHANGWE NA ZISIKIKE"
Tunamshukuru Mungu, siku ya leo tumekuwa na Tamasha kubwa la kusifu na kuabudu , lililobeba jina la "SHANGWE NA ZISIKIKE"
Timu ya waimbaji , ijulikanalo kama "WALAWI". Wakielekea madhabahuni.
Timu ya WALAWI, ikihudumu madhabahuni katika tamasha kubwa la kusifu na kuabudu
Pichani, ni Kwaya ya Vijana, ijulikanayo kama "GOOD NEWS BRINGERS", ikihudumu katika Tamasha kubwa la kusifu na kuabudu.
PICHANI: ni Mchungaji kiongozi wa kwaya ya WALAWI, akiwapongeza watu kwa kuhudhuria kwa wingi.
Pichani: Mchungaji kiongozi wa kanisa la Msewe Christian Revival Centre, Mchungaji Godwin Mujaki. akimuabudu Mungu katika Tamasha kubwa la Kusifu na Kuabudu.
Pichani: Mama mchungaji wa kanisa la Msewe Christian Revival Centre, Mama Mchungaji Scolla Mujaki. akimuabudu Mungu katika Tamasha kubwa la Kusifu na Kuabudu.
Pichani ni baadhi ya watumishi wa Mungu wakikemea pepo, katika Tamasha kubwa la Kusifu na kuabudu.
Hakika tulimuona Mungu katika tamasha hili, usikose kila jumapili kufika kanisani Msewe Christian Revival Centre.
WATU WOTE MNAKARIBISHWA.
Friday, September 8, 2017
TUITION YA WATOTO , BURE KILA JUMAMOSI
Wazazi na walezi, Tunapenda kuwakaribisha kuwaleta watoto katika Tuition inayofanyika kila siku za Jumamosi kuanzia saa tatu kamili asubui.
.
Masomo ya Tuition yanatolewa Bure, pia, Vyakula na Vinywaji vinagawiwa BURE kwa kila mwanafunzi.
.
Walengwa ni Wanafunzi wote wa chekechea na shule za msingi waliopo Dar Es Salaam.
.
Waalimu mahili kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salaam Pamoja na shule mbali mbali za msingi, wapo kuhakikisha mtoto wako anapiga hatua
.
Lengo la Tuition hizi, ni kuongeza viwango vya ufaulu mashuleni.
.
Ili kufika, panda magari ya kimara shuka kitu kituo kinachoitwa Rombo, kishaulizia, makanisa mawili, au Kanisa la TAG MSEWE
.
kwa Mawasiliano zaidi tuwasiliane 0752 636641
.
Watoto Wote Mnakaribishwa sana.
Wednesday, December 16, 2015
Subscribe to:
Posts (Atom)