UJAZO WA ROHO MTAKATIFU
Tunamshukuru Mungu Jumapili hii Mungu ameonekana kwa namna ya tofauti sana, Mchungaji Eliya lugwami alihubiri juu ya Roho Mtakatifu.Moja ya kitu alicho sema ni "Wajibu wa mkristo baada ya kumpokea Yesu kristo,ni kupokea Roho wa Mungu" hii ni kweli maana kama ilivyoandikwa katika kitabu cha " Matendo ya mitume 1: 8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi."
Roho Mtakatifu anakazi nyingi kwa mtu aliyeokoka, kama,
1. kututia nguvu/ kutuwezesha
2. Kutuongoza
3. Kutuchukua na kututia kwenye kweli yote
4. Kutukumbusha
5.Kutuombea
6. Kutuwezesha kujua tuliyo kirimiwa
7. Kutupasha habari ya mambo yajayo
pia unaweza ukapitia haya maandiko kwa uwelewa zaidi
No comments:
Post a Comment